Wanafunzi waandamana Chile

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanafunzi wa Chile wanafanya maandamano ya kutaka sekta ya elimu nchini humo kuimarishwa

Kumeshudiwa ghasia na fujo katika mji mkuu wa Chile, Santiago, kati ya polisi wa kupambana na ghasia na wanafunzi ambao wanataka mabadiliko makubwa yafanyiwe sekta ya elimu.

Wanafunzi hao wanataka kujumuishwa katika mabadiliko yanayofanyiwa mfumo wa elimu ya vyuo vikuu.

Wanafunzi hao wanaamini kuwa mfumo huo wa sasa unapendelea vyuo vikuu vya kibinafsi ilihali vyuo vikuu vya umma vikiachwa katika hali mbaya.