Aliye pandikizwa uume,baba mtarajiwa

Image caption Madaktari wakiwa katika chumba cha upasuaji

Daktari wa usapuaji nchini Afrika Kusini amethibitisha kwamba mwanamme wa kwanza aliyepandikizwa uume atakuwa baba hivi karibuni.

Professor Andre van der Merwe, ambaye ndiye aliyefanya upasuaji huo mwezi Disemba, ameiambia BBC kwamba mwenza wa mgonjwa huyo ana uja uzito wa miezi minne.

Mwanamme huyo mwenye umri wa miaka 21 alipoteza uume wake pindi alipokuwa anapashwa tohara ambayo haikufanikiwa.

Professor van der Merwe ameendelea kusema habari hizo zinaonyesha kuwa upandikizwaji huo wa kiungo umefanikiwa kabisa na unaweza kufanyiwa wagonjwa wengine katika siku zijazo.