Waasi wa Myanmar wasitisha vita

Haki miliki ya picha
Image caption Waasi wa Myanmar

Waasi katika jimbo la Kokang nchini Myanmar,ambao wamekuwa wakikabiliana na majeshi ya serikali wamesitisha mapigano.

Kupitia taarifa, kundi hilo la kikabila kutoka China, limesema kuwa linatazamia kuhusika pia katika shughuli za upigaji kura.

Katika kujitolea katika shughuli hizo, limeamua kuweka silaha chini na kukomesha mashambulizi hasa baada ya kushinikizwa na utawala wa Beijing.

Aidha, waasi hao wanasema kwamba wana haki ya kujilinda iwapo watashambuliwa na vikosi vya serikali ya Burma.

Mzozo huo m'baya uliodumu miezi minne sasa kati ya mataifa hayo mawili umeshuhudia makombora yakirushwa kutoka Burma na kuanguka ndani ya mipaka ya China huku uhusiano kati ya Beijing na Yangon ukiyumba.