Je,Australia huwahonga walanguzi wa watu?

Image caption Tony Abbot

Waziri mkuu wa Australia Tony Abbot hajapinga ripoti kuwa maafisa wake mpakani mwa taifa hilo waliwalipa walanguzi wa watu fedha ili kuirejesha mashua iliyokuwa imejaa wahamiaji hadi Indonesia.

Akijibu madai ya afisa mmoja mkuu wa polisi wa Indonesia, kwamba Australia iliwalipa walanguzi wawili dola elfu thelathini.

Haki miliki ya picha AFP GETTY IMAGES
Image caption Abbot

Bwana Abbot amesema kuwa, mikakati ya ubunifu inatumika ili kuzima mashua ya wahamiaji kuingia nchini humo.

Mwaandishi habari wa BBC mjini Sydney, anasema kuwa Australia imechukua uamuzi mgumu dhidi ya wahamiaji huku ikifanya kila mbinu kuzizuia mashua zinazowabeba wahamiaji kufika kwenye fukwe zake.