Mwanaharakati anayejifanya mtu mweusi

Image caption Dolezal

Wazazi wa mwanaharakati mmoja wa haki za raia nchini Marekani wamesema kuwa anajifanya kuwa mtu mweusi kwa miaka kadhaa sasa.

Rachel Dolezal analifanyia kazi shirika liitwalo National Association for the Advancement of Colored People {NAACP} huko Spokane takriban maili 280 mwa mji wa Seattle kazkazini magharibi mwa Marekani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ombi la kazi alilowasilisha Rachel linasema kuwa yeye ni mchanganyiko wa mtu mweupe na wa kihindi

Kulingana na msemaji wa gazeti la Review,Dolezal amesema kuwa yeye ni mchanganyiko wa mtu mweupe,mweusi na muhindi wa Marekani katika ombi lake alilowasilisha kwa tume ya polisi inayosimamia malalamishi ya raia mnamo mwezi Januari.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wazazi wa Dolezal ambao ni wazungu Ruthanne na Lawrence wamesema kuwa ni mwana wao wa kumzaa

Ombi hilo sasa linachunguzwa.

Meya wa mji wa Spokane David Condon na rais wa baraza la mji huo Ben Stuckart alitoa taarifa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bi Dolezal akishiriki maandamano na watu weusi

Kwa miaka mingi Rachel Dolezal anasema kuwa yeye ni mzaliwa mwenye mizizi ya Kiafrika na Marekani madai ambayo wazazi wake wamekana.

Nilikutana na Rachel Dolezal na sikuwa na wasiwasi kuhusu anakotoka.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Picha za awali na za sasa

Wazazi wa Dolezal ambao ni wazungu Ruthanne na Lawrence wamesema kuwa ni mwana wao wa kumzaa.