Waliopiga picha za uchi mlimani washtakiwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption mlima kinabalu

Watalii wanne ambao wamekiri kosa la kuonyesha matendo ya aibu hadharani, wamefikishwa katika mahakama moja nchini Malaysia.

Wanne hao ambao ni mawakala wa kupanga safari za kitalii walivua nguo na kubaki uchi kabla ya kujipiga picha juu ya kilele cha mlima wa Kinabalu.

Kwa mjibu wa watu wa Malaysia, mlima huo ni mtakatifu.

Sasa wanasubiri kuhukumiwa.

Baadhi ya raia wa Malaysia wamesema kuwa mitetemeko ya ardhi ya mara kwa mara nchini humo, inatokana na kusumbuliwa kwa mapepo yaliyoko huko.