Vita dhidi ya IS vyaigharimu Marekani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashambulizi yanayotekelezwa na Marekani na washirika wake dhidi ya wapiganaji wa IS

Marekani imetumia zaidi ya dola bilioni mbili unusu katika kufadhili vita dhidi ya Islamic State, kupitia kutekeleza mashambulizi ya angani nchini Iraq na Syria tangu mwezi Agosti mwaka jana.

Makao makuu ya Pentagon yametoa orodha ya gharama ya fedha zilizotumika, inayoonyesha kuwa inatumia zaidi ya dola milioni tisa kwa siku katika kutekeleza operesheni hiyo.

Bunge la Marekani limekataa jaribio la kuzuia matumizi zaidi ya fedha ili kukabiliana na IS.

Bunge la wawakilishi limepitisha mswaada wa kuikubalia wizara ya ulinzi kutumia dola bilioni mia tano na themanini.