Straus Kahn aondolewa mashtaka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyekuwa kiongozi wa hazina ya fedha dunia IMF

Kiongozi mkuu wa zamani wa shirika la fedha Duniani IMF, Dominique Strauss Kahn, ameondolewa mashtaka yote ya kujihusisha na makahaba kinyume cha sheria.

Mahakama iliyosikiliza kesi hiyo huko Ufaransa ndio iliyoondoa mashtaka hayo yaliyodai kuwa bwana Strauss Kahn, akishirikiana na watu wengine walikuwa wakiwatumia makahaba kufanya vitendo vya ufuska katika karamu za ulevi wa kupindukia lakini alijitetea kwa kusema hakujua wanawake hao walikuwa wanalipwa kufanya matendo hayo.

Jaji amesema ushahidi unaonyesha bwana Strauss Kahn alishiriki kama mteja na wala hakuwa miongoni mwa waliopanga matukio hayo.

Ni kesi ya miaka minne iliyofichua siri nyingi za yale yaliyokuwa yakiendelea katika karamu hizo za kashfa .

Hii inamaanisha bwana Khan ameondolewa pia lile shtaka la kumnyanyasa kimapenzi mwanamke mmoja mfanyikazi katika hoteli ya huko New york Marekani hapo 2011.