Walimu wakataa kurudi kazini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Shambuliz la Garissa

Walimu ambao walilitoroka eneo la kazkazini mashariki mwa Kenya wakihofia mashambulizi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Al shabaab wamekataa kurudi eneo hilo.

Mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay alielezea katika kipindi cha Newsday kwamba asilimia 60 ya walimu hawatoki katika eneo hilo na waliokwenda likizo wengi wamekataa kurudi.

Ameelezea kuwa takriban walimu 2000 wamelitoroka eneo hilo na kwamba nusu ya idadi ya shule za eneo hilo zimefungwa.

Amesema kuwa wafanyikazi wa uma pia wamelitoroka eneo hilo.