Bi Clinton ahutubia umma New York

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bi Clinton ahutubia umma New York

Mgombea wa kiti cha urais nchini Marekani bi Hillary Clinton amefanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara tangu atangaze nia ya kuwania kiti cha Urais.

Bi Clinton ambaye anapigiwa upatu wa kutwaa tikiti ya chama cha Democratic katika uchaguzi huo wa urais, ametangaza ruwaza yake mbele ya maelfu ya mashabiki wake mjini New York.

Wandani wa kampeini yake wanaazimia kuimarisha ushindani wake machoni mwa wapiga kura watakaomchagua atakayerithi kiti cha rais Obama.

Kulingana na kura ya maoni ushawishi wake umekuwa ukidorora tangu atangaze niya yake mwezi Aprili.

Bi Clinton alikuwa ameandamana na mumewe aliyekuwa rais wakati mmoja Bill Clinton na mwanaye wa kike Chelsea.

Haki miliki ya picha nc
Image caption Bi Clinton aliandamana na mumewe Bill na mwanawe Chelsea

Bi Clinton 67 alitoa video ijumaa hii akinadi sera zake kuwa zinalenga kutetea maslahi ya ''raia wa kawaida tu Mmarekani.''

''Kila mmoja wetu anahaki ya kupata maisha mazuri tu na kuishi kwa amani na ustawi kadri ya uwezo wake aliopewa na mwezi mungu''

''Hiyo ndiyo ndoto yangu hiyo ndiyo vita tunayopaswa kupigania ''alisema bi Clinton.

''Babangu mimi alikuwa mtoto wa mfanyikazi wa kawaida kiwandani aliyejikakamua na kuanzisha biashara ndogo''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Clinton anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Democratic

Mamangu pia japo hakuenda chuoni alinisomesha nikahitimu chuoni''

''Kila Mmoja wetu anahitaji kuwa na ndoto na mtu anayemuiga ambaye ameanzia chini maisha yake na kuimarika kufikia ufanisi wa kutajika ,alisema bi Clinton

Huu unatizamwa kama mwamko mpya katika kampeini ya bi Clinton.