Marekani yahamisha 6 kutoka Guantanamo

Haki miliki ya picha United States Department of Defense
Image caption Marekani yahamisha 6 kutoka Guantanamo

Marekani inasema kuwa imewaamisha wafungwa sita raia wa Yemen waliokuwa wamezuiliwa kwa miaka mingi katika gereza la Guantanamo kwenda nchini Oman.

Makao makuu ya jeshi la Marekani yametoa shukran kwa taifa hilo la ghuba katika kile yamesema kuwa ni ishara ya ubinadamu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani yahamisha 6 kutoka Guantanamo

Yameishukuru Oman kwa kujitolea kuunga mkono jitihada za marekani za kufunga gereza la Guatanamo.

Rais Obama alikuwa ameahidi kufunga gereza la Guantanamo wakati akifanya kampeni mwaka 2008 lakini hajafanya hivyo.

Hata hivyo utawala wake umepunguza idadi ya wafungwa kwa nusu.