Mgonjwa wa MERS alazwa Slovakia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mgonjwa wa MERS alazwa Slovakia

Mwanamme raia wa Korea Kusini ambaye anakisiwa kuambukizwa homa hatari ya MERS amelazwa hospitalini nchini Slovakia.

Ikiwa itabainika kuwa anaugua uugonjwa huo, kitakuwa kisa cha kwanza cha ugonjwa wa MERS kuripotiwa barani Ulaya tangu ugonjwa huo kuripotiwa nchini Korea Kusini mwezi uliopita.

Shirika la afya dunia limeutaja ugonjwa wa MERS kwa mkubwa. Litaandaa kikao cha dharura kuzungumzia ugonjwa huo siku ya Jumanne.

Hadi sasa watu 14 wameripotiwa kuaga dunia kutoka na homa ya MERS.