Uingereza yahamisha majasusi wake

Image caption Uingereza yahamisha majasusi wake

Afisi ya juu katika serikali ya Uingereza imeiambia BBC kuwa ililazimu majasusi wa Uingereza kuhamishwa kutokana na sababu kuwa Urusi na China zifanikiwa kupata taarifa za kisiri jinsi zinavyoendesha shughuli zake zilizoibiwa na jasusi raia wa marekani Edward Snowden.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Edward Snowden

Gazeti la Uingereza la Sunday Times linasema kuwa Urusi na China walidukua nyaraka kwenye mitandao. Serikali ya Uingereza inasema kuwa hakuna dalili kuwa udukuzi huo umesababaisha madhara yoyote.

Edward Snowden ambaye ni mwanakandarasi wa zamani katika shirika la ujasusi la marekani , aligonga vichwa vya habari miaka miwili iliyopita baada ya kifichua ujasusi wa mitandao na wa simu uliokuwa ukiendeshwa na Marekani na Uingereza. Kwa sasa anaishi nchini Urusi.