Aliyemuudhi Museveni aachiliwa Uganda

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aliyemuudhi Museveni aachiliwa Uganda kwa dhamana

Mkosoaji mkuu wa serikali ya Uganda kupitia mitandao ya kijamii, Robert Shaka,aliewekwa rumande wiki iliopita kwa madai ya kutumia vibaya mtandao wa kijamii ameachiliwa huru kwa dhamana hadi kesi yake itakapoanza kusikizwa mwishoni mwa mwezi huu.

Mwandishi wa BBC aliyeko Kampala Siraj kalyango na maelezo zaidi anasema kuwa Robert Shaka, aliyekamatwa wiki iliyopita na kufikishwa mahakamani kuhusiana na kesi ya matumizi mabaya ya mitandao.

Upande wa mshtaka unadai kuwa Robert Shaka anayetumia jina la badia katika ukurasa wa facebook la Tom Voltaire Okwalinga, alisambaza taarifa mbalimbali nyeti kwa usalama wa taifa na pia kutoa hali ya kiafya ya rais.

Lakini yeye amakanusha hayo na leo kupitia mawakili wake kuachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu millioni mbili za Uganda ambazo ni sawa na kama dola mia saba hiviā€¦.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bwana Shaka aliombwa kuacha mahakamani cheti chake cha kusafiria

Bwana Shaka aliombwa kuacha mahakamani cheti chake cha kusafiria .

Mmoja wa mawakili wake Issac Semakedde amefurahia hatua ya kumuachilia huru mteja wake kwa dhamana.

Robert Shaka anashtakiwa kutumia vibaya mitandao ya kijamii kinyume na kifungu namba 25 cha sheria ya matumizi mabaya ya kompyuta.

Image caption Sheria hiyo ilipitishwa mwaka wa 2011.

Sheria hiyo ilipitishwa mwaka wa 2011.

Ingawa mshukiwa amekana kosa hilo lakini upande wa mashtaka unasisitiza kuwa mshukiwa anahusika na kusema na kukusanya ushahidi wa kutosha kuhusu suala hilo.

Inadaiwa kuwa makosa yalifanyika kati ya miaka 2011 na 2015.

Kesi itaendelea June 30 mwaka huu.