Burundi tayari kwa Uchaguzi mkuu, Waziri

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Nkurunziza anawania muhula wa tatu

Huku ikiwa imesalia wiki chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Burundi vyama vya kisiasa vinaendelea na kampeini zao.

Serikali ya Burundi imeihakikishia jamii ya kimataifa kuwa hali ya usalama imeimarika baada ya maandamano ya upinzani kuzimwa.

Aidha serikali kupitia kwa waziri wake wa maswala ya kigeni ameiambia BBC kuwa mazingira yataruhusu uchaguzi huru na wa haki.

Image caption Serikali ya Burundi imeihakikishia jamii ya kimataifa kuwa hali ya usalama imeimarika baada ya maandamano ya upinzani kuzimwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi ameihakikishia jamii ya kimataifa kuwa taifa lake litaandaa uchaguzi huru na wa haki.

Akiongea wakati wa mkutano wa muungano wa Afrika nchini Afrika Kusini bwana Alain Aime Nyamitwe amesema kuwa hali ya kisiasa nchini humo imeimarika na vyama vyote kwa sasa vinaendelea na kampeini tayari ya kuchaguzi.

Kuhusiana na suala la waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa kususia uchaguzi huo, waziri huyo amekariri kuwa zoezi hilo linahusisha raia wa burundi na wala sio waangalizi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serikali inasema iko tayari kuandaa uchaguzi

Hata hivyo amesema kama taifa lolote huru, wao wametoa mwaliko kwa makundi yote na uamuzi ni wao ikiwa watakwenda Burundi au la.

Wakati huo huo amesema serikali ya rais Pierre Nkurunziza wako tayari kuendeleza mazungumzo ya viongozi wa upinzani ili kuwepo kwa uchaguzi huru na wa haki, ila tu ni wapinzani ndio wanaohujumu mpango huo.

Wakati huo huo rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonya wakuu wa serikali dhidi ya kuanzisha machafuko kwa kuwania zaidi ya mihula miwili.

Onyo hilo lilionekana kuelekezwa kwa rais wa Burundi ambaye anawania muhula wa tatu licha ya pingamizi kutoka kwa upinzani kuwa ametumikia mihula miwili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakimbizi zaidi ya laki moja wametoroka Burundi kwa hofu ya machafuko

Rais Nkurunziza amekariri kuwa muhula wa kwannza ulikuwa kipindi cha mpwito.

Rais mugabe anahudumu muhula wa saba lakini wa kwanza chini ya katiba mpa ya Zimbabwe, inayowashurutisha marais kuwania muhula miwili tu.

Wakati huo huo Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameshutumu mataifa ya magahribi kwa kushinikiza viongozi wa bara la Afrika kuhudumu mihula miwili pekee.