Mlima Everest ulisonga kufuatia tetemeko

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kambi iliyofunikwa na maporomoko ya theluji katika mlima Everest

Watafiti wa maswala ya ardhi kutoka China wanasema kuwa mlima Everest ulisongeshwa takriban sentimita tatu kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotikisa Nepal mwezi Aprili.

Hata hivyo watafiti hao wanasema kuwa mlima huo ungali kimo hicho hicho.

Takriban watu elfu nane waliangamia tetemeko hilo lililofika kipimo cha 7.8 kwenye mizani ya Richter lilipokumba eneo la mlima Everest.

Image caption Baadhi ya majumba yaliyoporomoka kufuatia tetemeko hilo kubwa Aprili

Tetemeko hilo lilisababisha maporomoko ya ardhi na theluji kutoka mlima huo mrefu zaidi duniani.

Ajabu ni kuwa sasa wanasayansi nchini Nepal na wanasema kuwa mji mkuu wa Kathmandu umesonga kwa zaidi ya mita mbili kuelekea Kusini.