NATO yaishutumu Urusi kutishia kijeshi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi, NATO

Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi, NATO umeishutumu Urusi kwa vitisho vya kijeshi baada ya Rais Vladimir Putin kutangaza mabadiliko ya kuimarisha silaha za nyuklia za nchi hiyo kwa kuweka makombora mapya arobaini ya masafa marefu.

Katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, ameitaja hatua hiyo ya Urusi kuwa ya hatari na inayoyumbisha mwelekeo.

Uamuzi wa Urusi unajibu mipango ya Marekani ya kujiimarisha kijeshi katika nchi za Ulaya Mashariki zilizo wanachama wa NATO.

Bwana Putin ameonya kuwa hatasita kulinda nchi yake.'Kama mtu yeyote anatishia baadhi ya maeneo yetu, kwa hiyo tutaelekeza majeshi yetu kufanya shambulio la kisasa kwa nguvu kutoka kule kunakotokea kitisho hicho. Hakuna njia nyingine', anasema Bwana Putin.