Ukusanyaji wa takwimu za HIV wapingwa

Haki miliki ya picha bbc
Image caption HIV

Mahakama kuu nchini Kenya inaendelea kusikiliza kesi iliyowasilishwa na wakereketwa wa haki za kibinadamu wakipinga mpango wa Serikali kukusanya takwimu za watoto wanaougua viini vinavyosababisha ukimwi, HIV.

Wakereketwa hao wanasema kuwa kuwekwa kwa takwimu hizo kunakiuka haki ya usiri ya watoto hao na wameomba mahakama kuwa takwimu zilizokusanywa kufikia sasa ziharibiwe.

Mnamo Februari, Rais Uhuru Kenyatta, alitoa amri kuwa takwimu zikusanywe za wote walio na virusi hivyo, kukiwemo wanawake waja wazito, ili kuhakikisha kuwa kuna mpango maalumu wa kupambana na maradhi hayo.

Zaidi ya Wakenya milioni moja nukta sita wana virusi hivyo vinavyosababisha ukimwi na karibu nusu milioni, kati yao ni watoto.