Roboti kuchukua kazi za raia Australia

Haki miliki ya picha
Image caption Roboti

Takriban asilimia 40 ya kazi nchini Australia ambazo zipo kwa sasa huenda zikapotea katika kipindi cha kati ya miaka 10 hadi 15 ijayo .

Ripoti mpya ya kamati ya maenedeleo ya kiuchumi CEDA imebaini kwamba matumizi ya mitambo inayojiendesha katika vizazi vijavyo inaweza kubadilisha nguvukazi ya taifa hilo.

Haki miliki ya picha
Image caption Roboti la muuguzi

Wimbi la mabadiliko ya kiteknolojia halipingiki na linafaa kuchukuliwa kama jeki ya kiuchumi.

Mitambo ya roboti inaweza kuchukua kazi zote kutoka uuguzi hadi upishi,udereva na kuwaosha wagonjwa wazee.

Image caption Roboti inayotengeza Sandiwichi

Katika maeneo mengine ya mashambani na majimbo ya Australia zaidi ya asilimia 60 ya kazi zinaweza kupotea kulingana na afisa mkuu wa CEDA Profesa Stephen Martin.