Viongozi wa Euro kuijadili zaidi Ugiriki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri wa Fedha wa Ugiriki Bwana Yanis Varoufakis

Viongozi wa kitaifa kutoka nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro wanatarajiwa kuwa na kikao cha dharura Jumatatu ijayo, baada ya kushindwa kwa jitihada za hivi karibuni za kutatua mgogoro wa deni la Ugiriki.

Mawaziri wa fedha wa nchi zinazotumia sarafu ya euro, baada ya mkutano wao nchini Luxembourg, wamesema hakuna maendeleo yoyote yaliyofikiwa katika suala la madeni na makataba wa Ugiriki kuhusu madeni hayo.

Ugiriki lazima ilipe deni lake kubwa kwa Shiriks la Fedha Duniani, IMF, kufikia mwishoni mwa mwezi huu la sivyo ikabiliwe na uamuzi wa kuitoa katika muungano wa nchi za Euro.

Waziri wa Fedha wa Ugiriki Yanis Varoufakis amesema aliwasilisha mipango ya kuinusuru nchi yake isiwe mufilisi, lakini amesema makubaliano yoyote yatakayofikiwa lazima yahusishe upunguzaji deni.