Aung Suu Kyi ataka uchaguzi wa haki

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Aung Suu Kyi

Aliyekuwa mfungwa wa kisiasa na ambaye sasa ni kiongozi wa upinzani nchini Myanmar, Aung San Suu Kyi, ametoa wito kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ufanywe kwa njia ya haki na ukweli.

Katika mkanda wa video uliowekwa kwenye mtandao katika kuadhimisha miaka 70 tangu azaliwe amesema matokeo ya uchaguzi, unaotarajiwa Novemba utaamua mwelekeo wa siku za usoni za taifa hilo.

Bi Suu Kyi ameishi muda mrefu wa miaka 25 iliyopita katika kifungo cha nyumbani, ingawa miaka mitatu iliyopita amekuwa mbunge.

Image caption Aung Suu Kyi

Alipowasili bungeni wabunge wenzake walimpa maua mekundu ya waridi kuadhimisha miaka 70 tangu kuzaliwa kwake.

Mwaka huu huenda ukawa muhimu sana katika maisha yake ambayo yamekuwa na panda shuka nyingi.

Mnamo Novemba chama chake cha kisiasa cha National League for Democracy kitashiriki katika uchaguzi wake wa kwanza kwa muda wa miaka 25.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aung Suu kyi

Iwapo chaguzi utakuwa wa haki inatazamiwa kuwa chama hicho kitashinda vyama vingi.

Kazi ngumu itaanza wakati huo iwapo chama chake kitashinda kwa sababu katiba kwa sasa haimruhusu kuwa rais kwa kuwa watoto wake ni raia wa Uingereza.

Ni wazi kuwa akitaka kutawala lazima atafanya mashauriano na wabunge na Jeshi, ambalo lingali na ushawishi mkubwa nchini humo.

Ushawishi mkubwa katika siasa za Burma umewekwa katika katiba na anaweza kuruhusiwa kutawala iwapo atamruhusu Jemedari mmoja kushikilia kiti cha juu Serikalini mwake iwapo anashinda.

Katika taarifa yake ya kanda ya vedio aliyoitoa kuadhimisha miaka ya kuzaliwa kwa dakika 10 Bi Sukyi amesema anatarajia kuishi kwa miaka mingine 90 na kuwa atashuhudia nchi hiyo ikiendelea kustawi.