Obama kuzuru nchini Ethiopia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Obama

Ikulu ya white house nchini marekani imetangaza kuwa rais wa Barack Obama atakuwa rais wa kwanza wa Marekani aliye madarakani kufanya ziara nchini Ethiopia.

Msemaji wake (Josh Earnest) alisema kuwa ziara hiyo itakuja baada ya ziara ambayo atafanya nchini Kenya ambapo ni nyumbani kwa babake akiwa rais wa marekani.

Ethiopia na Kenya zote zimekuwa kwenye mstari wa mbele katika vita dhidi ya kundi la Al Shabab nchini Somalia.