Philae Lander chatuma ujumbe tena

Haki miliki ya picha AFP ESA MEDIALAB
Image caption Philae Lander chatuma ujumbe tena

Chombo cha kwanza cha angani kutua kwenye kimondo kimefanya mawasiliano ya kwanza na kituo cha kukielekeza.

Shirika la safari za anga za juu barani ulaya, linasema kuwa chombo hicho kilituma ujumbe siku ya Ijumaa ukiwa ndio wa pili wiki hii baada ya miezi saba iliyopita

Chombo hicho kimefanikiwa kutuma ujumbe baada ya kuanza kukaribia miale ya jua ya kukiwezesha kupata nguvu.

Waelekezi wa safari saa juu sasa wanafanya jitihada za kuboresha uwezo wa chombo hicho.