Bunge la Afghanistan lashambuliwa

Image caption Bunge Afghanistan

Ripoti zinasema kuwa kumetokea mlipuko mkubwa karibu na bunge la Afghanistan huko Kabul .

Picha za runinga zinaonyesha wabunge wakikimbilia usalama wao.

Zipo ripoti zinazosema kuwa watu waliokuwa na bunduki walivamia jengo hilo.

Polisi wanajaribu kuwaondoa watu katika eneo hilo.

Kundi la Taliban limesema kuwa linajaribu kutekeleza mashambulizi hayo ili kusadifiana na kura ya kumwidhinisha waziri mpya wa ulinzi.