watu ishirini wafariki dunia Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maiduguri yashambuliwa

Watu ishirini wamefariki dunia kutokana na shambulio la kujitoa muhanga katika soko la wachuuzi wa samaki lililokuwa limefurika watu eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Watu wengi walikuwa wameumia vibaya wakati mwanamke mmoja alipojiripua kati kati ya watu katikati mwa mji wa Maiduguri.

Mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza kwamba mwanamke mwingine alijaribu kushambulia eneo hilo hilo kwa jaribio la kujilipua lililoshindwa,lakini baadaye aliamua kukimbilia msikitini,ambapo alikufa baadaye baada ya mabomu aliyojifungia kuripuka.

Mpaka sasa haijajulikana kwamba ni nani anayeendesha mashambulio hayo kati ya makundi ya kigaidi yakiwemo Boko Haram ambalo lina nguvu kubwa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria,ambapo mara kadha wamekuwa wakitumia watu wanaojitoa muhanga na vilipuzi.