Buhari awaonya viongozi dhidi ya ufisadi

Haki miliki ya picha Buhari Campaign
Image caption Rais Muhammadu Buhari

Rais mpya nchini Nigeria Muhammadu Buhari amewaambia magavana kuwa siku za matumizi mabaya ya fedha zimekwsha.

Buhari ambaye amekuwa uongozini chini ya mwezi mmoja amesema kuwa atafanya kila awezalo kurudisha mabilioni ya dola zilizoibiwa na maafisa wafisadi wa serikali zilizopita

Amesema kuwa nchi hiyo kwa sasa haina fedha kuongeza kuwa ni aibu kuwa wafanyikazi wa serikali hawalipwi.