Soko la Gikomba lachomeka Kenya

Image caption Gikomba

Soko kubwa la kuuza nguo kukuu nchini Kenya la Gikomba katika mji wa Nairobi limeteketea.

Moto huo ulianza mwendo wa saa kumi na moja asubuhi.

Kumekuwa na juhudi nyingi za kuzuia moto huo kusambaa hadi katika maeneo jirani.

Image caption Soko la Gikomba

Moshi ulionekana ukifuka kutoka mbali.

Baraza la jiji la Nairobi limekuwa mbioni kuzima moto huo ambao umesababisha hasara isiyoweza kukadiriwa.