Wanajeshi Wakurdi waiteka ngome ya IS

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Qurdi Syria

Wanajeshi wa Kikurdi kaskazini mwa Syria wanasema wameingia katika himaya ya Islamic State, na kuiteka ngome ya kijeshi katika mkoa wa Raqqa.

Eneo hilo lililokuwa limetekwa mwaka uliopita ni kilomita hamsini tu kaskazini ya pale wanapopaita makao ya wanamgambo hao katika mji wa, Raqqa.

Wanajeshi wa kikurdi walisaidiwa na mashambulizi ya angani na makundi mengine ya waasi nchini Syria.

Shambulizi hilo linafanyika wiki moja baada ya wapiganaji wa kikurdi kuteka mpaka wa Uturuki kutoka kwa wapiganaji hao.