James Horner afariki ajalini

Haki miliki ya picha epa
Image caption James Horner

James Horner, mtunzi nguli wa eneo maarufu kwa watu maarufu la Hollywood ambaye aliandika na kushinda katika tuzo za Oscar juu ya filamu maarufu ulimwenguni ya Titanic,amefariki dunia mjini California kutokana na ajali ya ndege akiwa na umri wa miaka 61.

James alipata mafunzo ya urushaji wa ndege,inaarifiwa alikuwa peke yake wakati alipopata ajali hiyo,na ndege binafsi ndogo ambayo alipata nayo ajali eneo la Kusini mwa Santa Barbara mwanzoni mwa wiki hii .

Mwandishi huyu na mtunzi wa tungo mbali mbali ametia mkono wake katika kazi tatu tofauti za filamu za msanii James Cameron , pamoja na filamu ya A Beautiful Mind, Braveheart, Troy na ile ya Apollo 13.katika utendaji kazi wake uliotukuka, James alipewa tuzo ya Oscar kwa filamu ya Titanic na wimbo uliotawala humo na nyinginezo .

James alipewa tuzo ya ushirika katika tuzo ya pili kwenye mashairi na msanii Will Jennings kwa wimbo bora wa asili , na kwa mafanikio makubwa waliyoyapata katika wimbo maarufu wa My Heart Will Go On, ambao uliimbwa na Celine Dion.

Ajali hiyo ilitokea katika msitu mzito wa taifa la Marekani wa Los Padres, Kaskazini mwa Los Angeles, wakati ndege hiyo ikidondoka ilitoa mshindo mkuu na kuripuka mara tu ilipotua aridhini moto ambao baadaye ulizimwa na kikosi cha wazima moto wa eneo hilo. Wanaeleza mashuhuda ambao ni wazima moto.

Msaidizi wa marehemu Horner , Sylvia Patrycja amethibitisha juu ya kifo hicho kwa kuandika kweny ukurasa wake wa facebook mwanzoni mwa wiki hii akisema kuwa: "tumempoteza mtu wa kipekee sana ambaye alikuwa na moyo mkuu wa kujitoa na mtu mwenye kipaji kisicho elezeka .amekufa wakati anafanya kitu akipendacho. Asante kwa mchango wako mkubwa na upendo uliokuwa nao tutaonana mbinguni ."