Malkia kuhama kasri la Buckingham

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kasri la Buckingham

Malkia 'huenda akaihama kasri yake ya Buckingham'

Aliyekuwa katibu wa zamani wa habari za kifalme Dickie Arbiter amesema kuwa malkia Elizabeth wa Uingereza atahama kasri yake ya Buckingham ili kutoa fursa kwa kazi ya kukarabati jengo hilo ambalo limeanza kuharibika.

Shughuli za ukarabati zitagharimu pauni milioni 150 za Uingereza.

Mojawepo ya mapendekezo ya jamii ya kifahari ni kuwa, kasri hiyo inahitaji kuwekwa upya mifereji ya kupitishia maji pamoja na maji taka, nyaya zote za umeme zinafaa kutolewa na kuwekwa mpya na pia mapambo hayajafanyika tangu mwaka 1952.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Familia ya Ufalme

Haya yanajiri baada ya kampuni ya Crown Estate, ambayo inamiliki rasilimali kwa niaba ya malkia, iliporejesha faida ya pauni milioni 285 fedha ya walipa ushuru mwaka jana na kufikisha kiwango hadi asilimia 6 nukta 7.

Ufadhili wa malkia unatarajiwa kupanda kwa pauni milioni mbili mwaka ujao na kufikia pauni milioni 42 nukta 8.

Mwaka jana, malkia alipata pauni milioni 37 nukta 9 kutoka katika hazina hiyo ambapo alitumia pauni milioni 35 nukta 5.

Kiwango hicho kitapanda na kufikia pauni milioni 40 nukta 05 mwaka huu.