Polisi awa 'baba' kufuatia ajali

Image caption Polisi awa baba baada ya ajali

Afisa mmoja wa polisi nchini Marekani alilazimika kuwa mzazi baada ya kumpata mtoto akiwa hai kufuatia ajali mbaya iliyosababisha kifo cha babake.

Mauti yaliikumba familia hiyo ya baba mama na watoto wanne mjini Colorado Marekani.

Hata hivyo mtoto wao wa miaka miwili alinusurika bila hata ya kuchubuka !

Mtoto huyo wa kike alipatikana na makundi ya waokoaji akiwa analia huku babake akiwa ameaga dunia kufuatia ajali hiyo.

Mamake na ndugu zake 3 walikuwa wamejeruhiwa vibaya sana.

Waokoaji walimpokeza mtoto huyo afisa wa polisi aliyekuwepo huku wakiendelea kuwaokoa jamaa zake.

Afisa huyo wa polisi alilazimika kutumia ujuzi wake kama mzazi kumtuliza.

Alimuimbia,akambembeleza na hata akamuhadithia ilimradi tu kumtuliza.

''Twinkle Twinkle Little Star''alimuimbia mtoto.