Ulaya na Ugiriki zimetofautiana zaidi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mazungumzo kati ya Ugiriki na wafadhili kutoka Ulaya yamekamilika

Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schaeuble ameonya kuwa tofauti iliopo kati ya Ugiriki na wakopeshaji wake wa kimataifa inazidi kuongezeka.

Mawaziri wa fedha wa mataifa ya bara Ulaya wanaokutana mjini Brussels kwa mara ya nne katika kipindi cha wiki moja, wanasema kuwa Ugiriki imerudi nyuma zaidi.

Katika mkutano wa awali na Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras, wakopeshaji walipendekeza kupunguzwa kwa malipo ya uzeeni na kuondoa ushuru mdogo kwa raia walioko katika visiwa vya Ugiriki.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waziri Tsipras amekataa kata kata kupunguza malipo ya uzeeni akisema itawadhuru raia wa kawaida

Waziri Tsipras amekataa kata kata kupunguza malipo ya uzeeni akisema itahujumu uwezo wa Wagiriki ambao hawana kitega uchumi kuendelea kujikimu kimaisha.

Awali Mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Bara Ulaya walikutana kutafuta mbinu ya kuisaidia Ugiriki.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras na wakopeshaji kutoka bara Ulaya

Shirika la fedha Duniani- IMF, linataka serikali ya Ugiriki ambayo ilipendekeza kukata matumizi ya fedha na kuongeza ushuru Jumatatu na kupunguza matumizi zaidi kabla ya kuokolewa.

Athens, inahitaji msaada wa kifedha kulipa madeni yake kufikia mwisho wa mwezi huu.