Watu 37 wameuawa hotelini Tunisia

Haki miliki ya picha tv
Image caption Runinga ya taifa imepeperusha picha za shambulizi hilo

Watu wenye silaha wameshambulia hoteli moja ya kitalii iliyoko kwenye pwani ya Tunisia na kuwauwa watu 37.

Maafisa wa serikali ya Tunisia wamesema kuwa mmoja wa washambuliaji hao aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa ulinzi na kuwa waliosalia bado wanasakwa na polisi.

Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Sousse, ambao huwavutia maelfu ya watalii kutoka bara Ulaya na Afrika ya Kaskazini.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wa polisi wanasema kuwa mmoja wa magaidi hao ameuawa

Hili lilikuwa shambulizi la pili dhidi ya hoteli ya watalii nchini Tunisia katika kipindi cha miezi michache iliyopita.

Inaaminika kuwa washambuliaji hao waliwavamia watalii ufukweni.

Mnamo mwezi Machi mwaka huu, wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwauawa zaidi ya watu 26 katika makavazi ya Bardo, iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo Tunis.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Watu 27 wameuawa hotelini Tunisia

Makavazi hayo ya Bardo hilo lilikuwa maarufu sana kwa watalii.

October mwaka wa 2013, mlipuaji wa kujitoa, alijilipua nje ya nyumba moja mjini Sousse, baada ya maafisa wa polisi kutibua jaribio lake la kutaka kuingia ndani na kuishambulia.