Islamic State watimuliwa kutoka Kobane

Haki miliki ya picha Sedat Suna EPA
Image caption Islamic State watimuliwa kutoka Kobane

Wapiganaji wa Kikurdi Kaskazini mwa Syria wanaripotiwa kuwatimua wapiganaji wa kundi la Islamic State kutoka mji wa Kobane.

Shirika la haki za binadamu lenye makao yake nchini Uingereza lilisema kuwa wapiganaji wakurdi kwa mara nyingine wamechukua udhibiti wa mji wa Kobane baada ya mapigano makali.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanamgambo wa Islamic State walifanikiwa kuingia mji huo baada ya kufanya shambulizi la ghafla mapema siku ya Alhamis

Wanamgambo wa Islamic State walifanikiwa kuingia mji huo baada ya kufanya shambulizi la ghafla mapema siku ya Alhamis ambapo waliripotiwa kuwaua karibu watu 200 wakati wa uvamizi huo.

Serikali ya Syria imetoa wito kwa wenyeji kwenye mji ulio kaskazini wa Hassakeh kuulinda mji huo kutoka kwa wanamgambo wa islamic state.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Serikali ya Syria imetoa wito kwa wenyeji kwenye mji ulio kaskazini wa Hassakeh kuulinda mji huo kutoka kwa wanamgambo wa islamic state.

Kwenye ombi lililofanywa kwa njia ya runinga waziri wa habari alitoa wito kwa kila kijana wa kike na kiume aliye na uwezo wa kubeba silaha kutangulia vitani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiganaji wa Islamic State Raqaa

Alisemaa kuwa wanamgambo wa Islamic Sate waliharibu sehemu ya jengo la ulinzi ambapo watu kadha waliuawa

Wanamgamo hao walifanya uvamizi siku ya alhamisi na kufanikiwa kuteka sehemu ya mji huo.