Misikiti 80 kufungwa Tunisia

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Misikiti minane kufungwa Tunisia

Utawala nchini Tunisia unasema kuwa utafunga misikiti 80 katika kipindi cha wiki moja inayokuja kwa madai ya kuhubiri chuki na jihad.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Zaidi ya watalii 2500 kutoka Uingereza wametoroka na kurejea makwao

Hii ni kufuatia shambulizi lililofanyika kwenye hoteli moja hapo jana ambapo takriban watu 39 wengi wao wakiwa raia wa mataifa ya ulaya waliuawa na mwanamme mmoja aliyejifanya kuwa mtalii.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Asili mia kubwa ya wahasiriwa wa mkasa huo ni raia wa Uingereza

Wapiganaji wanaoshirikiana na wanamgambo wa Kundi la kiislamu la Islamic State wamesema kuwa wao ndio waliotekeleza shambulizi hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Miili ya watalii ilikuwa imetapakaa ufukweni

Waziri mkuu nchini Tunisia Hanib Essid anasema kuwa misikiti hiyo ndio iliokuwa ikitumika kueneza propaganda na kuunga mkono ugaidi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu ametangaza kuwa misikiti hiyo ndiyo imekuwa ikihubiri Jihad

Hali ya usalama umeimarishwa maradufu katika maeneo mengi mjini Tunis na karibu na majengo yenye watalii wengi.

Haki miliki ya picha
Image caption Mpiganaji mmoja alijifanya kuwa mtalii kabla ya kuwafyatulia risasi watalii ufukweni

Tayari wanajeshi wa akiba wameamrishwa kuripoti mara moja katika kambi za jeshi zilizoko karibu nao.