Wanawake 2 wajitoa mhanga Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanawake 2 wajitoa mhanga Nigeria

Wanawake wawili washambuliaji wa kujitoa mhanga wamewaua takriban watu watatu kwenye shambulizi katika mji wa Maiduguri ulio kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wanawake hao walijaribu kuingia kwenye hospitali lakini wakasimamishwa na walinzi langoni ambapo walijilipua.

Watu wengine 16 walijeruhiwa.

Shambulizi hilo ndilo la hivi punde kati ya mashambulizi yanayoendeshwa na wanamgambo wa Boko Hara.

Rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari ameufanya mji wa Maiduguri kuwa kituo cha kijeshi kuweza kupambana na Boko Haram.