Sam Smith na Nicki Minaj wang'ara BET

Image caption Sam smith

Sam Smith ameshinda tuzo la msani bora mpya katika tamasha la mwaka huu la tuzo za BET mjini Los Angeles.

Hatahivyo hakuwepo katika sherehe hizo na hivyobasi tuzo lake likachukuliwa kwa niaba yake na nyota wa uigizaji Anthony Anderson.

Image caption Nicki Minaj

''Sam Smith hayupo hapa usiku huu kwa kuwa yeye ni mzungu na hakufikiria kwamba angeshinda katika tuzo za BET ''aliuambia umati mkubwa katika ukumbi wa Los Angeles.

''Hakufikiria kwamba angeshinda Lakini tumemuonyesha kwamba tunampenda''.

Image caption Terrence Horwad

'Nicki Minaj' ambaye alishinda tuzo lake la sita la msanii bora wa kike wa mtindo wa Rap mfululizo aliwasili katika jukwaa na mamaake.

Aliwasalimia wasanii wenzake wa muziki wa Rap walioteuliwa kugombea tuzo la Rap, Dej Loaf na mpenziwe Meek Mill ambaye aliketi karibu naye kabla ya kujiunga naye katika jukwa kwa onyesho la muziki wake.

''Mama nataka kukushukuru kutoka moyoni mwangu kwa kile kitu ulichonifanyia '',nakupenda sana alisema.

Image caption bet

Nicki Minaj pia alishinda tuzo la wimbo uliowavutia watazamaji wengi uliowashirikisha wasanii Drake,Lil Wayne na Chris Brown.

Akiimba juu ya gari la polisi lililokuwa na bendera ya Marekani ikipepea nyuma yake nyota wa muziki wa Hip Hop Kendrick ndio aliyeanzisha tamasha hilo.

Terrence Howard ,nyota wa msururu wa filamu ya Empire alishinda tuzo la muigizaji bora kwa kuigiza kama Lucious Lyon.

Image caption Chris Brown

''Taji hili nalitoa kwa Empire.Namshkuru Taraji P Henson kwa kumjali nduguye''.

Wakati huohuo Taraji P Henson alishinda tuzo la muigizaji bora wa kike kwa kuigiza kama Cookie Lyon katika filamu ya Empire.

Chris Brown alifanya wimbo wake katika jukwaa mara kadhaa na kushinda tuzo mbili kama msanii bora wa muziki wa R & B

Haki miliki ya picha b
Image caption Janet Jackson

Janet Jackson pia alijishindia tuzo licha ya kuwa anatarajiwa kutoa albamu mpya kabla ya kufanya ziara maeneo kadhaa duniani.