Lupita:Najivunia nywele zangu asili

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Muigizaji nyota mshindi wa tuzo la Oscar kutoka Kenya bi Lupita Nyon'go amesema kuwa anajivunia kuwa mwanamke mwenye nywele asili.

Muigizaji nyota mshindi wa tuzo la Oscar kutoka Kenya bi Lupita Nyon'go amesema kuwa anajivunia kuwa mwanamke mwenye nywele asili.

Lupita alisema kuwa licha ya kushamiri katika kilele cha anga za sanaa huko Holywood Lupita anasema anajivunia nywele zake asili.

Image caption Lupita alipotua Hollywood

Lupita ambaye hunyoa nywele zake na wala hatumii dawa na kemikali za kunyosha nywele hizo anasema ''kama mwanamke mwafrika hana sababu ya kuaibikia muonekano wake asili''

''Nilihisi kama mtu aliyefunguliwa baada ya kukata nywele zangu zilizokuwa na kemikali ama ''perm''

Image caption Lupita akizungumza na mwandishi wa BBC mjini Nairobi Kenya Anne Soy.

Lupita alikuwa akizungumza na mwandishi wa BBC mjini Nairobi Kenya Anne Soy.

Bi Nyong'o aligonga vichwa vya habari aliposhinda tuzo la Oscar kufuatia mchango wake katika filamu ya ''12 years a Slave''.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Lupita alivuma katika filamu ya ''12 years a Slave''

kwa sasa anaigiza katika filamu ya ''Americanah'' ambayo iliandikwa na msanii Chimamanda Ngozi Adichie kutoka Nigeria.

Mojawepo ya mada kuu katika riwaya hiyo ni siasa za nywele.

Image caption lupita ametajwa kuwa balozi wa mazingira wa WildAid Wildlife

Kwa sasa bi Nyon'go aliyeteuliwa kuwa balozi wa maswala Mazingira wa shirika lisilokuwa la serikali la WildAid wildlife yuko nchini Kenya kuhamasisha umma kuhusu kazi hiyo yake mpya.