Waasi na jeshi wapambana,Sudan Kusin

Image caption Salva Kiir Rais wa Sudan Kusini

Kikosi cha waasi Sudan Kusini na majeshi ya serikali wamepambana kuwania kumiliki mji wa Malakal, Jimbo la Kaskazini,kama njia ya kufikia jimbo la Upper Nile eneo lililo na mafuta.

Mji wa Malakal unaendelea kubadilika tangu miezi kumi na nane ya mapigano kati ya serikali na waasi wanaomuunga mkono makamu wa Rais wa zamani Riek Machar.

Pande zote mbili ziliweza kukutana na Rais Uhuru Kenyatta wa kenya siku ya jumamosi, na kuwataka kusitisha mapigano.