Warundi 10,000 wakimbia nchi wikendi

Wakimbizi wa Burundi
Image caption Raia wengi wa Burundi wameendelea kukimbia nchi

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa{UNHCR} linasema karibu raia 10,000 wa Burundi walikimbia nchi hiyo wikendi iliyopita kabla ya uchaguzi wa ubunge.

UNHCR inasema baadhi ya watu walilazimishwa nje ya mabasi walipojaribu kuondoka nchini.

Wengi walilazimika kutembea kwa muda murefu wakipitia vichakani kuepuka polisi na makundi ya sugusungu.

Haki miliki ya picha
Image caption UNHCR inasema Warundi 10,000 wamekimbia nchi wikendi iliyopita

Umoja wa Mataifa unaongeza kwamba idadi kubwa ya watu waliokimbia walisema nchi hiyo inakumbwa na msukosuko mkubwa wa kisiasa.

Zaidi ya raia laki moja wa Burundi wamekimbia nchi hiyo tangu mwezi Aprili wakati kulizuka ghasia kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.