Al Sisi aapa kuzima ugaidi Misri

Mashambulizi Misri Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashambulizi yameongezeka nchini Misri tangu kuondolewa kwa Mohamed Morsi

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ameapa kuweka sheria kali kukabiliana na ugaidi, siku moja baada ya mkuu wa mashtaka ya umma kuuawa mjini Cairo.

Kwenye hotuba iliyopeperushwa kwa runinga wakati wa mazishi ya Hisham Barakat, Bw Sisi alisema haki haiwezi kamwe kukandamizwa na sheria. Alipendekeza haja ya kuweka marekebisho ya katiba kuhakikisha haki inatekelezwa kwa haraka.

Haki miliki ya picha afp getty
Image caption Hisham Barakat aliuawa kwenye shambulio la bomu mjini Cairo hapo Jumatatu

Bw Barakat ndiye afisa wa juu zaidi serikalini kuuawa tangu makundi ya wapiganaji kuimarisha mashambulio dhidi ya maafisa wa usalama Misri.

Mashambulio yamekithiri baada ya kuondolewa kwa Rais aliyeegemea mrengo wa kidini Mohamed Morsi miaka miwili iliyopita.