Mashambulio mabaya Misri

Rasi ya Sinai Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rasi ya Sinali imeshuhudia mashambulizi ya kila mara

Makundi ya wapiganaji yamefanya misururu ya mashambulio dhidi ya maafisa wa usalama nchini Misri katika Rasi ya Sinai.

Jeshi limesema makabiliano yanaendelea huku wanajeshi kadhaa na wapiganaji wakiuawa.Taarifa ya jeshi imesema vizuizi vitano vya polisi vililengwa sawa na kituo kimoja cha polisi.

Image caption Wapiganaji wa Kiisilamu wamekuwa wakiwalenga wanajeshi

Hili ndilo shambulio kubwa zaidi kufanywa na wapiganaji wa kiisilamu walioko eneo la Sinai, miaka miwili baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais aliyeegemea mrengo wa kidini Mohamed Morsi.

Tukio hili limejiri siku moja baada ya Rais wa Misri Abdul Fattah al Sisi kuapa kupendekeza sheria mpya za kukabiliana na ugaidi. Hapo Jumatatu mwendesha mashtaka wa Misri aliuawa katika shambulio la bomu iliyotegwa ndani ya gari.