Ugiriki yalegeza kamba kupata fedha

Alexis Tsipras Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri Mkuu wa Ugiriki amelazimika kulegeza kamba kuunusuru uchumi wa nchi yake

Ugiriki inasema kwamba itakubali mapendekezo ambayo wakopeshaji wake waliwasilisha wikendi iliyopita lakini kwa masharti fulani.

Hata hivyo Ujerumani imepuzilia taarifa hiyo na kusema Ugiriki haina nia ya kujadili uzito wa mzozo wa sasa. Pendekezo la Ugiriki lilitolewa kabla ya siku ya mwisho ambapo ilishindwa kulipa deni lake.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Ugiriki imekubali mapendekezo ya wakpoeshaji wake japo kwa masharti

Masoko ya fedha yameimarika kufuatia taarifa hiyo. Mawaziri wa fedha kutoka kanda inayotumia sarafu ya Euro wanatarajiwa kuja dili mapendekezo hayo baadaye.

Mikutano ya leo itaangazia ombi la Ugiriki kupata mkopo wa dharura. Aidha kuna pendekezo zaidi ambapo Ugiriki inaomba fedha zaidi kuuchepua uchumi wake. Katika kipindi cha miaka miwili, Ugiriki imepokea mkopo wa Euro bilioni 29.1.