IS yashambulia polisi Misri

Rasi ya Sinai imelengwa na wapiganaji wa kiisilamu Haki miliki ya picha na
Image caption Rasi ya sinai imelengwa na wapiganaji wa kiisilamu

Wapiganaji wa Islamic State wamefanya misururu ya mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama nchini Misri katika Rasi ya Peninsula.

Jeshi linasema makabiliano bado yanaendelea.Duru za usalama zinasema kwamba watu 50 wameuawa.

Mmoja wa wanaoshuhudia matukio haya ameambia BBC kwamba wapiganaji wameingia katika barabara za mji wa Sheikh Zuwaid.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption haya ndiyo mashambulio mabaya zaidi kuwahi kulenga maafisa wa usalama

Taarifa ya jeshi imesema vizuizi vitano vya polisi vililengwa sawa na kituo cha polisi. Hili ndilo shambulio baya zaidi ambalo limefanywa na wapiganaji wa kiisilamu yakilenga maafisa wa usalama.

Ni mashambulio makali kuwahi kutekelezwa tangu kuondolewa kwa Rais aliyeegemea mrengo wa kidini Mohamed Morsi miaka miwili iliyopita.

Shambulio la leo limejiri siku moja baada ya Rais wa Misri Abdul Fattah al Sisi kuapa kuweka sheria ili kukabiliana vikali na makundi ya wapiganaji.

Hapo Jumatatu mwendesha mashtaka wa Misri aliuawa kwenye shambulio la bomu.