Ghadhabu baada ya wauaji kuachiwa huru

Mwanamama Farkhunda
Image caption Farkhunda alipigwa mawe kwa kisingizio kwamba aliiteketeza Koran

Makundi ya kutetea maslahi ya wanawake yameghadhabishwa na mahakama ya rufaa nchini Afghanistan ambapo imebatilisha hukumu ya kifo dhidi ya wanaume wanne waliohusika na mauaji ya mwanamke mjini Kabul mwezi Machi.

Wakili wa familia ya mwanamke huyo amelalamikia mahakama hiyo kwa kuendesha uwamuzi wake faraghani. Naye kakake marehemu amesema uwamuzi huo ni ukiukaji mkubwa wa haki.

Haki miliki ya picha
Image caption Wanaume wanne walikua miongoni mwa waliompiga mawe hadi kufa Farkhunda

Mwanamke huyo kwa jina Farkhunda, alishambuliwa katika msikiti mmoja baada ya kutuhumiwa bila ukweli kwamba aliiteketeza Koran. Alipigwa mawe hadi kufa, maiti yake ikakanyagwa kwa gari na kisha ikateketezwa.

Mahakama ya rufaa pia imemuachia huru msimamizi wa msikiti huo.