Mihadhara ya 'La' na 'Ndio' Ugiriki

Waandamanaji Ugiriki Haki miliki ya picha AP
Image caption Serikali imewaomba raia kusela 'La' kupinga masharti ya wakopeshaji wake

Kambi hasimu nchini Ugiriki zinatarajiwa kufanya mikutano mikubwa ya hadhara mjini Athens kabla ya kura ya Maamuzi hapo Jumapili, kuamua masharti ya kupokea mkopo kutoka kwa wakopeshaji wa kimataifa.

Waziri Mkuu Alexis Tsipras anatarajiwa kuongoza mkutano wa mrengo wa 'La' ambao unapinga masharti ya kupewa ufadhili.

Viongozi wa Muungano wa Ulaya wameonya kura ya 'La' huenda ikapelekea Ugiriki kuondoka katika kanda inayotumia sarafu ya Euro.

Ugiriki imeshindwa kuafikiana na wakopeshaji wake kwa miezi kadhaa na ililazimika kuitisha kura ya maamuzi wiki jana. Kila upande umekua mbioni kupata eneo la mkutano wake mjini Athens.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kila upande utafanya mkutano mkubwa mjini Athens

Mikutano yote itafanyika kati kati mwa Athens kila upande ukijaribu kuwashawishi wafuasi wake kuhusu kura hii ya maamuzi.

Kumekuwa na maandamano kadhaa katika siku za karibuni baadhi yakikumbwa na vurugu kati ya waandamanaji na polisi.

Wakati huo huo mahakama ya juu Ugiriki inatarajiwa kuamua ikiwa ni halali kura hiyo kufanyika siku ya Jumapili.