Mazungumzo ya Iran yaendelea Austria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mazungumzo ya Iran yaendelea Austria

Wapatanishi wa kimataifa wanaendelea na mazungumzo na Iran mjini Viena nchini Austria yenye lengo la kuafikia makubaliano kuhusu mpango wa nuklia wa nchi hiyo.

Awali waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Iran Javad Zarif alisema kuwa Iran itashirikiana na nchi za magaharibi kupambana na wanamgambo wa islamic state ikiwa makubaliano yataafikiwa kuhusu mpango wake wa nuklia.

Matamshi yake yalitolewa kupitia ujumbe uliowekwa kwenye mtandao wa YouTube wakati mazungumzo yanapoendelea mjini Vienna kuafikia makubaliano ya kimataifa.

Afisa kutoka nchini marekani hata hivyo alisema kuwa licha ya kundi la islamic state kuwa adui wa kila mtu mazungumzo ya Vienna yanalenga hatari inayotokana na mpango wa nuklia wa Iran.