Mmiliki na nahodha wa ferry mahakamani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mmiliki na nahodha wa ferry mahakamani

Polisi nchini Ufilipino wamewafungulia mashtaka mmiliki na nahodha wa ferry ambayo ilizama siku ya Alhamis na kuwaua zaidi ya watu 50.

Wahudumu 17 wa ferry hiyo nao wamekamatwa.

Wachunguzi wanaamini kuwa ferry hiyo huenda ilibeba watu wengi kuliko kiwango inachostahili ikiwa pia na mizigo.

Ferry hiyo ilipinduka muda mfupi baada ya kuondoka katika bandari ya Ormoc kati kati mwa ufilipino.

Mmiliki wa ferry hata hivyo amekana madai kuwa ilikuwa na watu wengi kuliko kiwango inachotakiwa.