Mji wa Bujumbura
Huwezi kusikiliza tena

Viongozi EAC waijadili Burundi

Mawaziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki wamekutana jijini Dar es Salaam mapema wiki hii, kujadili ripoti mbili za Timu ya Kimataifa ya Usuluhishi wa mgogoro wa Burundi, ya Joint International Facilitation Team, na ile ya baraza la mawaziri wa Afrika Mashariki wakati wakuu wa nchi za Afrika Mashariki nao wanatarajiwa kukutana pia mjini Dar es Salaam kujadili hali ya kisiasa nchini Burundi.

Kufuatia hali hiyo mwandishi wa BBC Regina Mziwanda alizungumza na mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar-Es-Salaam ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania Bashiru Ally, kutaka kujua kutoka kwake kwamba huu si mkutano wa kwanza kufanyika, maazimio yalishapitishwa awali sasa, nini kitafanyika ili Rais Pierre Nkurunziza aheshimu mkutano huu?