Mazungumzo ya Iran kuendelea Austria

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Mazungumzo ya Iran kuendelea Austria

Mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni wanaoshiriki kwenye mazungumzo ya mpango wa nuklia wa Iran wanatarajiwa kurudi mjini Vienna hii leo kutafuta kuafikia makubaliano.

Mawaziri hao watashiriki mazungumzo makubwa yenye lengo la kuafikia makubaliano ya mwisho ifikapo siku ya jumanne.

Iran na mataifa mengine sita makubwa duniani wanasema kuwa wanakaribia kuafikia makubaliano lakini kuna maswala tata yanayostahili kusuluhishwa.

Tarehe za mwisho za kuafikiwa makubaliano mara nyingi zimeshindikana lakini Iran ina haja ya kuondolewa vikwazo na mataifa ya magharibi ambayo pia yanataka kuhakikisha kuwa Iran haitaunda silaha za nuklia.